Asenali Yabanduliwa na Baselona kwa Ligi Ya Mabingwa Barani Ulaya

Kocha wa Asenali Arsene Wenger amesema timu ya Baselona ina wachezaji wawili au watatu mahiri walio na uwezoA� wa kufanya maisha ya kawaida kuwa kama sarakasi.

Asenali ilibanduliwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya katika awamu ya timu 16 bora baada ya kushindwa na Baselona kwa jumla ya mabao matano kwa moja.

WachezajiA� watatu mahiri katika kikosi cha Baselona, Lionel Messi, Neymar Junior na Luis Suarez walitikisa wavu kila mmoja.

Kwenye mechi nyingine iliyochezwa jana usiku, Bayern Munich ya Ujerumani ilitoka nyumaA� na kuishinda Juventus.A� Huku timu hizo zikiwa sare mabao mawili kwa mawili kufuatia matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza, Paul Pogba na Juan Cuadrado waliiweka Juventus kifuambele.

Lakini bao la Robert Lewandowski kwa kichwa liliirejeshea Bayern matumaini huku Juventus ikijiandaa kutwaa ushindi hadi wakati Thomas Muller alipopachika bao katika dakika ya tisini na kulazimisha mechi kuingiaA� muda wa ziada ambapo Thiago na Kingsley Coman waliifuzisha Bayern Munich kwa robo fainali ya kipute cha ligi ya mabingwa Barani Ulaya.