Arsene Wenger kuchezesha wachezaji wake dhidi ya Bate Borisov

Kocha wa timu ya Asenali, Arsene Wenger, atawachezesha wachezaji wake wazoefu dhidi ya Bate Borisov usiku huu uwanjani Emirates, licha ya kuwa tayari timu hiyo inaeongoza kundi a�?Ha�� la ligi ya Yuropa. Asenali imefuzu kwa awamu ya 32 bora bilaA�A�kuwatumia wachezaji wake mahiri. Olivier Giroud, Jack Wilshere na Theo Walcott hawajaanza mechi ya ligi kuu nchini Uingereza msimu huu, lakini wameshirikishwa katika ligi ya Yuropa. Asenali ikiwa tayari imefuzu kwa raundi ya 32 bora, Bate Borisov ya Belarus ni mojawapo ya timu tatu zinazowania nafasi ya pili ya kufuzu kundini humo. Borisov, iliyoshindwa na Asenali nyumbani mabaoA�A�manne kwa mawili, mwezi September, inavuta mkia kundini, alama moja nyuma ya Red Star Belgrade na Cologne, zitakazocheza usiku huu nchini Serbia katika mechi ya pili ya kundi a�?Ha��.