Arsene Wanga apata afueni

Kocha wa Asenali, Arsene Wenger, alipata afueni ya kushutumiwa janaA� usiku baada ya timu hiyo kujipatia ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi yaA� AC Milan, katika mechi ya mkondo wa kwanza wa mchujoA� ya ligi ya Yuropa.

Bao lililofungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya 15 liliiweka Asenali kifua mbele kisha Aaron Ramsey akaongeza la pili muda mfupi kabla ya kipindi cha mapumziko. Wenge alikuwa akihitaji ushindi kufuatia shinikizo la kumtaka anga��atike wadhifani baada ya timu hiyo kuandikisha matokeo duni kwa kushindwa katika mechi nne mfululizo. Asenali, ambayo iko nyuma ya timu inayoongoza katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa alama 13, ina matumaini ya kuendeleza ushindi huo ili irejee katika ligi ya kilabu bingwa Barani Ulaya kwa kunyakua taji ya a�?Yuropaa�� kwa mara ya kwanza.