Arsenali yapata pigo kubwa mikononi mwa Bayern

Arsenali kwa mara nyingineA�A�imepata pigo kubwa katika awamu ya timu kumi na sita bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kunyukwa na Bayern Munich kwenye mechi ya mkondo wa kwanza nchini Ujerumaini. Timu hiyo ambayo imebanduliwa kwenye awamu hiyo katika kipindi cha misimu sita iliyopita , mara mbili na Bayern MunichA�A�ilifungwa mabao matano huku wenyeji wakitawala mchuano huo kwa zaidi ya asilimia sabini na tano. Alexis Sanchez,A�A�aliisawazishia Arsenali baada ya winga mahiri Arjen Robben kufunga bao kutoka yadi ishirini na tano.A�A�Mlinzi wa kutegemewa wa ArsenaliA�A�Laurent Koscielny alijeruhiwa katika kipindi cha pili huku Bayern ikifunga mabao zaidi kupitia kwa mshambulizi Robert Lewandowski na kiungoA�A�Thiago Alcantara. Mchezaji wa akiba , alipachika kimiani bao la tano. Kwenye mechi nyingine, Real Madrid iliishinda Napoli mabao matatu kwa moja.