Arsenal yabandua Sunderland Uingereza

Kimataifa, timu inayoshiriki kwenye ligi kuu ya soka nchini Uingereza Asenali ilihakikisha kuwa timu nne za mwanzo ligini zitabainikaA� wakati wa mechi za mwisho msimu huu baada ya kuishinda Sunderland, ambayo tayari imeshushwa ngazi, mabao mawili kwa bila uwanjaniA� Emirates, jana usiku.

Alexis Sanchez alipachika kimiani bao la kwanza baada ya kuunganisha krosi kutoka kwa kiungo Mesut Ozil na kuhuisha matumaini ya mashabiki wachache waliojitokeza uwanjaniA� Emirates.A� Aidha, Sanchez aliongeza bao la pili na kuimarisha matumaini ya Asenali ya kumaliza miongoni mwa timuA� nne za mwanzo katika kipindi cha takriban miongo miwili.A� Asenali iko alama moja nyuma ya Liverpool iliyo na ubora wa mabao mawili zaidi kabla ya mechi za mwisho Jumapili hii. Kikosi hicho cha kocha Arsene Wenger ni lazima kiishinde Everton Jumapili hii, nayo Liverpool ishindwe naA� Middlesbrough ili imalize miongoni mwa timu nne za mwanzo liginiA� Uingereza msimu huu.