Amnesty International-Mauaji Ya Kinyama Ya Watu 60 Sudan Kusini Ni Uhalifu Wa Kivita

Mauaji ya zaidi ya wanaume sitini na vijana kwa kuwafungia kwenye konteina moja hadi wakakosa hewa nchini Sudan kusini ni uhalifu wa kivita,haya yamesemwa leo na shirika la Amnesty International.Kwenye ripoti inayoeleza uhalifu huo uliotekelezwa na wanajeshi wa serikali kwa mara ya kwanza , shirika hilo la kutetea haki za binadamu lilitoa wito wa kushtakiwa kwa wahusika.Mauaji hayo ambayo serikali imekanusha yalitekelezwa kwenye eneo la kanisa moja katoliki mjini Leer mwezi Oktoba mwaka 2015.Kisa hicho kiliripotiwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita.Ripoti hiyo ya shirika la Armnesty inazingatia ushahidi wa watu 23 waliowaona wanaume hao na vijana wakilazimishwa kuingia kwenye konteina hiyo wakiwa wamefungwa mikono na wengine kuona miili ya watu hao.Kiwango cha joto kaskazini mwa nchi hiyo hufikia hadi nyuzi 40.Jamaa wa waliouawa wamesema jamaa wao walikuwa wafugaji, wafanyibiashara na wanafunzi na wala hawakuwa wapiganaji.