Anne Waiguru achaguliwa kuwania kiti cha ugavana Kirinyaga

Aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru ameshinda kwenye kura za mchujo za chama cha Jubilee  huko Kirinyaga ambapo sasa  atawania wadhifa wa gavana. Mpinzani wake wa karibu  ambaye  ni mbunge wa Kirinyaga ya kati  Joseph Gitari alipata kura 46,678 ikilinganishwa na kura 100,632 za Waiguru.Gavana wa sasa Joseph Ndathi alishika nafasi ya tatu kwa kura 11,556.Awali,Ndathi alilalamika kuhusu jinsi shughuli nzima ya uteuzi ilivyoendeshwa na kutaka irudiwe.