Ann Waiguru ashinda kesi iliyowasilishwa kupinga uchaguzi wake

Mahakama kuu huko Kerugoya imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kiongozi wa chama cha Narc-Kenya Martha Karua, kupinga uchaguzi wa gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru . Mahakama ilisema kuwa Karua hakuwasilisha matokeo ya uchaguzi huo yanayozua utata, pamoja na tarehe matokeo hayo yalitangazwa na tume ya uchaguzi-IEBC,ambazo ni hitaji msingi kwenye kesi hiyo.Akitoa uamuzi huo,jaji Lucy Gitari alisema Karua hakuzingatia kanuni za mwaka 2017 kuhusu uwasilishaji kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi .

Waiguru alikuwa amewasilisha ombi la kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali tarehe 17 mwezi uliopita kwa msingi wa kutotimiza kanuni zilizowekwa kisheria kupitia mwanasheria Kamotho Waiganjo. Karua amesema atawasilisha rufaa dhidi ya uamuzi huo,na kutaka akabidhiwa nakala zilizosainiwa za jinsi kesi hiyo ilivyoendeshwa.

A�