Amadou Gon Coulibaly amfuta kazi Massandje Toure Litse mkurugenzi mkuu wa kilimo

Waziri mkuu wa Ivory Coast Amadou Gon Coulibaly, amemfuta kazi mkurugenzi mkuu wa baraza linaloshughulikia maswala ya kilimo cha kahawa na Cocoa – (CCC), Massandje Toure Litse, kufuatia mzozo kuhusu ukiukaji wa mashartiA� ya kandarasi na maswala mengine ya usimamizi. Mshauri wa zamani wa Rais, Yves Kone ameteuliwa mkurugenzi mkuu mpya wa baraza la (CCC), wadhifa ambao ni mojawapo muhimu zaidi kwenye taifa hilo linalo-ongoza kwa uzalishaji Cocoa duniani, kulingana na vidokezi vya wizara ya fedha na pia baraza hilo la (CCC) kwa shirika la habari la Roita. Waziri mkuu Amadou Gon Coulibaly anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi huo wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri hivi leo. Sekta ya CocoaA� nchini Ivory Coast imeghubikwa na msururu wa mizozo mwaka huu, baada ya uvumi eti bei zingeendelea kupanda kukosa kudhibiti bei ya zao hilo hadi kufurikwa kwa masoko. Baraza hilo la (CCC) lilishtumiwa kwa kuchangia tatizo hilo.