Allen Gichuhi achaguliwa kuwa rais wa chama cha wanasheria

Allen Gichuhi alichaguliwa jana kuwa rais mpya wa chama cha wanasheria hapa nchini-LSK baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu James Mwamu. Gichuhi alipata kura-2,675 naye Mwamu akapata kura- 2,145. Gichuhi amechukua hatamu hiyo kutoka kwa Isaac Okero ambaye amekuwa rais wa chama hicho kwa muda wa miaka miwili iliyopita. Uchaguzi huo ulisimamiwa na maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC katika majengo-28 ya mahakama kote nchini. Kiti cha makamu wa rais kilivutia wagombeaji wawili wakuu  ambao ni James Mwamu na Joy Masinde. Hiyo ni mara ya  tatu kwa Mwamu kugombea kiti hicho baada ya kushindwa na aliyekuwa rais wa chama hicho Kenneth Akide mwaka-2010 na baye Kenneth Akide mwaka-2016. Gichui amewania kiti hicho kwa mara ya pili. Mawakili wengi baru baru walisusia uchaguzi huo wakisema sharti la kuwa na tajiriba ya miaka-15 kwa wagombeaji urais wa chama hicho na kiti cha naibu rais  halifai. Wakili wa Nairobi Nelson Havi alipinga bila mafanikio uamuzi wa kumzuia kugombea kiti cha urais wa chama cha LSK. Aliyekuwa mbunge maalum, Judith Sijeny ambaye pia alikuwa akiwania kiti hicho alijiondoa kwenye kinyang’anyiro