Aliyekuwa waziri mkuu wa Misri Ahmed Shafiq akana madai kuwa alitekwa nyara

Aliyekuwa waziri mkuu wa Misri A�Ahmed Shafiq amefanya mahojiano ya simu ya moja kwa moja kwenye runinga huku akikanusha madai ya kuwa alitekwa nyara. Familia ya A�Shafiq ilikuwa imeelezea wasiwasi hasa baada ya kushindwa kuwasiliana naye baada yake kuwasili nchini humo. Alirejeshwa nyumbani kutoka jamhuri ya milki za kiarabu siku jumamosi baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka mitano. A�Haya yanawadia baada ya Shafiq kuelezea nia ya kuwania urais nchini humo mwaka ujao. A�Alisema katika mahojiano hayo kuwa alikuwa anatafakari upya uamuzi huo. A�Wakili wake A�Dina Adly alitoa taarifa fupi akisema kuwa alikutana naye katika hoteli moja jijini Cairo. Shafiq alitorokea katika milki za kiarabu baada ya kushindwa katika uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2012 na A�Mohammed Morsi ambaye alitoa kibali cha kukamatwa kwake kuhusiana na madai ya ufisadi.