Aliyekuwa rais wa Korea Kusini Lee Myung-bak aanza kutumikia kifungo cha miaka-15 gerezani

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini, Lee Myung-bak ameanza kutumikia kifungo cha miaka-15 gerezani kutokana na mashtaka ya ufisadi.

Lee ambaye alikuwa rais kati ya mwaka-2008 na 2013, ni rais wa nne wa zamani wa Korea kusini kufungwa jela baada ya mtangulizi wake,Park Geun-hye¬† ambaye anatumika kifungo gerezani kwa kutokanana kashfa za ufisadi zilizosababisha ang’atuliwe mamlakani mapema mwaka-2017.

Geun-hye alifungwa pamoja na mkuu wa kampuni ya Samsung, Jay Y Lee. Myung-bak yasemekana alikubali hongo ya dola milioni-10 kutoka taasisi kadhaa ikiwemo kampuni ya Samsung na idara ya upelelezi, jambo lililovuruga uhusiano kati ya serikali na jamii ya wafanyabiashara.

Hata hivyo, Lee aliye na umri wa miaka-78 alikanusha mashtaka hayo akisema yalichochewa kisiasa na rais wa sasa.