Aliyekuwa mshauri wa Trump ashatakiwa kwa ulanguzi wa pesa

Wachunguzi wa kashfa ya Russia kuingilia mchakato wa uchaguzi wa urais wa MarekaniA� wameshitakiA� Paul ManafortA� ambaye alikuwa kiongozi wa kampeini za rais Donald Trump na mpambe wake Rick Gates kwa kosa la ulanguzi wa pesa. Aliyekuwa mpambe wa Trump,George Papadoupolous, mapema mwezi wa oktobaA� alipatikana na hatia ya kusema uwongo kwa shirika la ujasusi la Marekania��FBI.

Harakati hizo zote ni za miezi mitano za wakili mahususi wa idara ya haki ya Marekani Robert Mueller za uchunguzi kuhusu madai ya Russia kuingilia uchaguzi wa urais wa Marekani ikitumia wapambe wa Trump ambaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi huo. Wakili huyo aliamuru kutiwa nguvuni kwa washukiwa hao wawili na kumwachilia Manafort kwa dhamana ya dola milioni 10 na nyingine ya dola 5 kwa Gates.