Aliyekuwa mshambulizi wa timu ya Naijeria, Yakubu astaafu

Kimataifa, aliyekuwa mshambulizi wa timu ya Naijeria, Yakubu Ayiegbeni, amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 35.Baada ya kucheza kwa muda wa miaka kumi nchini Uingereza, baina ya mwezi Januari mwaka 2003 na Juni mwaka 2012, Yakubu alifunga mabao 114 katika mechi 293 nchini humo. Aidha,angefunga bao katika kila mechi akizichezea timu za Portsmouth, Middlesbrough, Everton, Leicester na Blackburn kabla ya kujiunga na kilabu cha Guangzhou nchini Uchina. Mchezaji huyo alirejea nchini Uingereza kwa muda mfupi na kuvichezea vilabu vya Reading mwaka 2015 na Coventry City. Yakubu alifunga jumla ya mabao 95 katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza zaidi ya mchezaji mwengine yeyote wa Naijeria na Didier Drogba, aliyekuwa mfungaji bora wa Afrika nchini Uingereza kwa muda wa miaka 25, alifunga mabao tisa pekee zaidi ya Yakubu.