Aliyekuwa mbunge wa Bomachoge Borabu, Joel Onyancha ameaga dunia

Aliyekuwa mbunge wa Bomachoge Borabu, Joel Onyancha ameaga dunia. Kwa mujibu wa familia yake, Onyancha alifariki akipokea matibabu kwenye hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Onyancha aliwania kiti cha bunge cha Bomachoge Borabu kwa tiketi ya chama cha Jubilee kwenye uchaguzi wa mwezi agosti lakini akashindwa na mwaniaji huru, Zadock Ogutu. Hata hivyo Onyancha alikuwa amewasilisha rufaa kupinga kushindwa kwake.