Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Panama Manuel Noriega aaga dunia

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa Panama, Manuel Noriega ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 83. Noriega alitawala taifa la Panama tangia mwaka 1983 hadi 1989 aliponga��atuliwa mamlakani na Marekani. Noriega amekuwa akipata matibabu tangu mwezi Machi mwaka huu kutokana na kuvuja kwa damu kwenye ubongo baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kwenye ubongo. Katika miaka ya awali ya utawala wake, Panama na Marekani zilikuwa washirika wa karibu lakini uhusiano huo ulizorota na kusababisha kunga��olewa kwake mamlakani.