Aliyekuwa Katibu Wizara Ya Utalii Rebecca Nabutola Na Mwenyekiti Wa Zamani Wa Bodi Ya Utalii Washindwa Kwenye Rufaa Dhidi Ya Hukumu Yao

Aliyekuwa katibu katika wizara ya utalii Rebecca Nabutola na mwenyekiti wa zamani wa bodi ya utalii hapa nchini, Achieng Onga��onga��a wameshindwa kwenye rufaa dhidi ya hukumu yao kwao kwa madai ya kuilaghai wizara hiyo zaidi ya shilingi-milioni 8. Mahakama badala yake imeagiza walipe faini ya shilingi nusu milioni kila mmoja au wafungwe kwa mwaka mmoja gerezani. A�Walikabiliwa na madai ya kukosa kuzingatia utaratibu wa ununuzi wa bidhaa. Hata hivyo mashtaka dhidi yao yaliondolewa na Grace Macharia. Hata hivyo mshtakiwa mwenzao Duncan Muriuki ambaye ni mhudumu wa watalii ndiye aliyepata ushindi mkubwa katika rufaa hiyo baada ya kuachiliwa huru na jaji huyo alipoamua kwamba upande wa mashtaka haujathibitisha madai dhidi yake. Maafisa hao wa serikali pamoja na mhudumu huyo wa utalii walishtakiwa mwezi Mei mwaka 2009 kufuatia mapendekezo ya iliyokuwa tume ya kukabiliana na ufisadi ambayo kwa sasa ni tume ya maadili na kupambana na ufisadi.Zamani