Aliyekua rais wa Korea Kusini afikishwa mahakani

Aliyekuwa rais wa Korea Kusini Geun-hye amefikishwa mahakamani kwa kosa la ufisadi,kwenye tukio la hivi punde kumkumba mwanassiasa huyo ambayo anakabiliwa na mzozo.Mwanasiasa huyo alifikishwa mahakamani akiwa amefungwa pingu mkononi.Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Geun-hye kufikishwa mahakamani tangu alipotiwa nguvuni mnamo mwezi wa Machi.Hata hivyo Pak amekanusha madai ya utoaji rushwa,kuvujisha siri za taifa na kutumioa vibatya mamklaka yake.Kiongozi huyo alishitakiwa kufwatia maandamano makubwa yaliofanywa nchini Korea kusini kulalamikia uongozi mbaya na amekuwa kizuizini tangu wakati huo.Bi.Pak alikuwa na umaarufu mkubwa alipochaguliwa kwa kura nyingi mnamo mwaka wa 2012.Kiongozi huyo anadai kuwa hana kosa lolote na kwamba anasingiziwa.Adhabu ya makosa yanayomkabili Bi.Pak ni kifungo cha maisha.Kuondolewa kwake mamlakani kulisababisha kuandaliwa mapema kwa uchaguzi wa urais ambapo Moon-Jae alichaguliwa kuwa rais.