Algeria yazima mitandao ya kijamii ili kuzuia wizi wa mitihani

Algeria imezima mitandao yake yote ya kijamii wakati huu wa mitihani ya muhula ya shule za upili katika juhudi za kuzuia visa vya udanganyifu. Mitandao ya kijamii, ikiwemo huduma za internet, rununu na simu tuamaa zilizimwa na zitasalia zikiwa zimezimwa hadi mitihani ya stashahada ya shule za upili itakapokamilika. Mitihani hiyo inafanywa kati ya tarehe 20 hadi 25 ya mwezi huu.

Haya yanajiri kufwatia  kukithiri kwa visa vya udanganyifu wakati wa mitihani kama  hiyo ya mwaka jana, ambapo maswali yalivujishwa mitandaoni  kabla ya tarehe za mitihani. Waziri wa elimu  Nouria Benghabrit alisema mtandao wa Facebook utafungwa kote nchini humo kwa kipindi hicho kizima. Aidha vifaa vyote vya elektroniki vilivyo na uhusiano na mitandao ya kijamii vitazimwa na havitatumiwa na wanafunzi na hata walimu. Wanafunzi pia hawataruhusiwa  kuingia  majumba 2,000 ya mitihani wakiwa na vifaa vya  elektroniki, ambapo pia watapekuliwa kabla ya kuingia kwenye vyumba vya kufanyia mitihani.