Aladwa Awasilisha Ombi La Kupinga Kushtakiwa

Aliyekuwa meya wa Nairobi George Aladwa amewasilisha ombi la kupinga kushtakiwa kwake kwa kosa la kuchochea ghasia.Aladwa ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa tawi la Nairobi la chama cha ODM kupitia kwa wakili wake John A�Khaminwa anadai kwamba taarifa ya mashtaka yake ina kasoro. Khaminwa aliiambia mahakama moja ya Nairobi kwamba taarifa hiyo ya mashtaka ilitiwa saini na maafisa wa polisi ambao sasa wameondolewa mamlaka ya kushtaki.Pia anasema taarifa hiyo iliyo mahakamani haikutiwa sahihi na mkurugenzi wa mashtaka ya umma jinsi inavyohitajika kisheria.Mwanasiasa huyo aliiomba mahakama hiyo imuondolee mashtaka hayo A�kwa misingi kwamba yanaenda kinyume cha katiba A�na hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki.Kwenye kesi hiyo, Aladwa amekanusha kutoa matamshi ya kuchochea ghasia endapo kiongozi wa upinzani Raila Odinga hatashinda urais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Anadaiwa kutoa matamshi hayo kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa Kibera zaidi ya mwaka mmoja uliopita.Kesi hiyo itatajwa jumatano wiki ijayo.