Al shabaab Washambulia Kituo Cha Polisi Mandera

Habari kamili kuhusu shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na washukiwa wa kundi la Al Shabaab katika kituo kimoja cha polisi huko Arabia, Mandera A�bado hazijatolewa huku idara ya polisi ikisema imepeleka maafisa zaidi wa polisi A�kuimarisha usalama katika eneo hilo. Kufikia sasa, habari zinaarifu kwamba kisa hicho kilichotokea mwendo wa saa nane alfajiri huenda kimesababisha vifo vya maafisa kadhaa wa usalama na kuwajeruhi wengine. A�Kamanda wa kaunti ya Mandera, Bernard Nyakwaka amesema hakujakuwa na mawasiliano kamili baina yao na maafisa katika kituo cha polisi wa utawala cha Arabia kilicho umbali wa kilomita-70 kutoka mjiniA� A�Mandera baada ya majambazi hao kudaiwa kukatiza vifaa vya mawasiliano kambini humo, hali iliyoathiri mawasiliano kati ya kambi hiyo na kambi nyingine za polisi. Wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab katika kipindi cha miezi michache iliyopita, wametekeleza mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki na kisa cha leo kimejiri miezi michache baada ya kundi hilo la kigaidi la Somalia kutekeleza shambulizi lingine huko Mandera, na kuharibu vifaa vya mawasiliano.A� A�