Ajali Ya Treni Yaua Watu Takribani Kumi Nchini Ujerumani

Watu wapatao kumi waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya treni mbili za abiria kugongana katika jimbo la Bavariaa nchini Ujerumani.

Ajali hiyo ilitokea karibu na eneo la A�Bad Aibling ambao ni kilomita 60 kusini mashariki ya jiji la Munich. Waziri wa uchukuzi nchini humo amesema kuwa treni hizo mbili zilikuwa zikiendeshwa kwa kasi ya kilomita mia moja kwa saa.

Makundi ya kushughulikia mikasa ya dharura yalikuwa yakifanya kila juhudi kuwaokoa manusura kutoka kwa mabaki ya treni hizo