Ajali ya ana kwa ana Pakistan yasababisha vifo vya watu 20

Ajali ya A�ana kwa ana ambayo ilihusisha Bus-dogo na Lori kusini mwa Pakistan imesababisha vifo vya watu 20 na wengine watatu kujeruhiwa hivi leo. Hatibu wa polisi Rab Nawaz alisema Lori hilo la mizigo liligonga Bus la abiria katika barabara moja ya sehemu za mashambani karibu na mji wa Khairpur. Awali duru za polisi ziliarifu kwamba watu 17 waliuawa lakini watatu zaidi walifariki baadaye wakati wa kupewa matibabu. Nawaz alisema kwamba wengine waliojeruhwia wako katika hali mahututi na kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka. Ma-dereva wa magari yote mawili ni miongoni mwa A�waliofariki. Uchunguzi wa awali ulionyesha kwamba mwendo wa kasi pamoja na ukungu wa nyakati za asubuhi ndio ulisababisha ajali hiyo. Nawaz A�alisema kwamba juhudi za kuondoa miili ya wahasiriwa zilitatizika kwaniLori hilo lilipinduka baada ya mgongano, na kulalia Bus hilo la abiria. Ajali za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Pakistan kwa ajili ya hali mbovu ya barabara na kupuuzwa kwa sheria za barabarani miongoni mwa Ma-dereva..