Ajali mbaya yatokea katika barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi

Mtu mmoja amefariki kufuatia ajali iliyohusisha ma-Lori mawili kwenye barabara kuu ya Mombasa kuelekeaA�A�Nairobi. Duru za polisi zimearifu kwamba, dereva wa mojawapo ya ma-Lori yaliohusika kwenye ajali katika eneo la milima ya Kyulu alichomeka hadi kufa, huku watu wengine watatu wakipata majeraha mabaya. Lori moja lililokuwa limebeba Gesi ya kupikia kutoka Mombasa; lili-lipuka kutokana na kishindo, baada ya kugongana ana kwa ana na Lori jingine. Awali waendeshaji magariA�A�kutoka Nairobi kuelekea Mombasa walishauriwa kubadili mkondo wao huko Emali na kutumia barabara ya Loitoktok – Taveta hadi Voi; Ilhali wale waliokuwa safarini kutoka Mombasa kuelekea Nairobi walikuwa wameshauriwa kubadili mkondo wao huko Voi na kutumia barabara ya Taveta- Loitoktok- hadi Emali. Sehemu ya barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi ilikuwa imefungwa kufuatia ajali hiyo ya mwendo wa saa nane usiku na ambayo ilipelekea kufungwa kwa safu zote mbili za barabara naA�A�kusababisha msongamano mkubwa wa magari