Ajali Barabarani Eneo La Sagaa

salgaa-A�

Watu wawili wameaga dunia na wengine watano kujeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea leo asubuhi katika taasisi ya mafunzo kwa walimu ya Nakuru karibu na eneo la Salgaa, kaunti ya Nakuru.

Akithibitisha kisa hicho, afisa mkuu wa trafik katika eneo la Rift Valley, Joseph Muthee alisema matatu iliyokuwa ikitoka Nakuru kuelekea Kisumu iligonga lori lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kukumbwa na kasoro za kimitambo.

Inadaiwa dereva wa matatu hiyo alipoteza mwelekeo na kugonga lori hilo upande wa nyuma ambapo watu wawili wakifariki papo hapo na wengine kadhaa waliojeruhiwa wakipelekwa katika hospitali ya Nakuru level five.

Ajali hiyo imejiri huku mwenyekiti wa bodi ya utoaji leseni za uchukuzi, John MututhoA�akiishutumu halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalaja barabarani kwa kutowajibika.A�A�Eneo la Salgaa hushuhudia ajali nyingi na serikali imekuwa ikishinikizwa kuchukua hatua.