Agizo la kukamatwa kwa Babu owino laondolewa

Agizo la kukamatwa kwa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino limeondolewa. Hakimu mkuu mwandamizi Martha Mutuku ameondoa agizo hilo baada ya mahakama kufahamishwa kuwa Owino alikosa kufika mahakamani kwa sababu alikuwa akishughulikia swala jingine. Kwenye kesi hiyo , Owino na mlinzi wakeA� Fanuel Owino walishtakiwa kwa kumshambulia mhudumu wa eneo la kuegeshea magari katika eneo la Westlands jijini Nairobi na kumsababishia madhara ya kimwili.Kesi hiyo itasikizwaA� tarehe 19 mwezi huu. Na mahakama kuu ya Kisii imepuuza rufaa ya kupinga uchaguzi wa Prof. Sam Ongeri kuwa seneta wa kaunti yaA� Kisii kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka uliopita. JajiA� Winfridah OkwanyiA�A�amedumisha ushindi wa Ongeri kwa misingi kuwa mlalalamishi hajathibitisha kuwa visa vya udanganyifu vilivyoshuhudiwa kwenye uchaguzi huo viliathiri matokero yote ya uchaguzi huo jinsi ilivyotangazwa na tume ya IEBC.A� Kwenye rufaa hiyo wapiga kura Charles Orito na Geroge Ogake wamedai kuwa tume ya IEBC haikutumia sajili ya kuaminika ya wapiga kura kutekeleza shughuli hiyo .A� A�A�A�