Afueni kwa seneta Linturi baada ya kesi yake kusimamishwa

Ni afueni kwa seneta wa Meru Mith ika Linturi baada ya mahakama kuu kusimamisha kwa muda kukamatwa kwake kwa kuhusiana na vyeti ghushi vya masomo,hadi kesi amewasilisha mahakamani itasikizwa na kuamuliwa. Linturi alikwenda mahakamani kutafuta agizo la mahakama kuzuia kukamatwa na kushtakiwa kuhusiana na shahada ghushi. Chuo kikuu cha Nairobi kilifutilia mbali usajili wake mwezi disemba mwaka uliopita siku chache kabla ya kufuzu na kufutilia mbali shahada yake ya sheria baada ya madai kuwa aliwasilisha stakabadhi ghushi wakati aliposajiliwa mwaka 2014. Linturi anasema alijiunga na chuo kikuu cha NairobiA�A�tarehe 3 mwezi januari mwaka 2014 alikuwa afuzu disemba 22 mwaka uliopita na shahada katika sheria .Anadai kuwa masaibu yake yalianza wakati wapinzani wake waliapa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa hawanii kiti hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka uliopita