Afisa Wa Polisi Na Raia Mmoja Wauawa Kwenye Maandamano Kongo

Afisa wa polisi na raia mmoja waliuawa wakati maelfu ya raia wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walipoandamana dhidi ya uongozi wa rais Joseph Kabila. Shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo limesema wawili hao waliuawa katika mji wa mashariki wa Goma. Katika mji mkuu, Kinshasa, maafisa wa usalama walifyatua vitoa machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanaji. Polisi walisema hata ingawa waandamanaji walikuwa na idhini ya kufanya hivyo, walitumia njia ambazo hawakuruhusiwa. Wafuasi wa kabila wanataka uchaguzi kuahirishwa kwa kati ya miaka miwili na miaka minne kutokana na changamoto za kiufundi na kifedha lakini upinzani unamshutumu kabila kwa kujaribu kufanyia katiba marekebisho ili kujiongezea muda wa kutawala.