Afisa wa polisi amwua mpenziwe Naivasha

Maafisa wa polisi wanaohudumu katika kituo cha polisi cha Kongoni huko Naivasha wamepigwa na butwaa baada ya mmoja wao kumuua mpenziwe kwa kumpiga risasi baada ya kulumbana naye. Afisa huyo amempiga risasi mara sita tumboni mwanamke huyo ambaye wamekaa pamoja kwa miaka miwili akitumia bunduki aina ya AK47 kabla ya kupokonywa bunduki hiyo na kukamatwa. Wakati wa kisa hicho cha jana usiku , mshukiwa huyo aliyetamnbulishwa kamaA�A�Benjamin Lelemen alimpiga risasi tumboni na kwenye mapajaA�A�Beatrice Nyokabi mwenye umri wa miaka 31 na kumuua papo hapo. Kisa hicho kimejiri wiki mbili baada ya afisa mwingine wa polisi kumuua naibu afisa mkuu wa polisi katika kituo cha polisi cha Makueni na kuwajeruhi wengine wawili.

Kwenye kisa cha Naivasha afisa huyo alikuwa ameingia kwenye nyumba walimokuwa wakiishi na mpenziwe wakati walipozozana. Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Naivasha Joseph Opondo amesema mshukiwa amehamishwa hadi katika kituo cha polisi cha Naivasha. Opondo ambaye anasimamia kituo cha polisi cha Kongoni ameongeza kuwa maafisa wanaofanya upelelezi wamepata bunduki iliyotumika katika mauaji hayo.