AFC Leopards Yanuia Kumsajili Mshambulizi Wakati wa Uhamisho Ujao

Kocha wa timu ya AFC Leopards amekiri kuwa ananuia kumsajiliA� mshambulizi mwengine wakati wa uhamisho wa wachezaji utakapowadia.

Mkufunzi huyo Raia wa Ubelgiji, amesema ushambulii wa timu yake ni butu kwani inawategemea sana washambulizi wawili; Kepha Aswani na Lamine Diallo, jambo ambalo haliridhishi kwa timu inayowania kutwaa taji ya ligi kuu ya Sportpesa humu nchini msimu huu.

Minnaert amesema nia yake kuu ni kumaliza miongoni mwa timu tatu bora wakati mechi za mkondo wa kwanza zitakapokamilika. Zipo tetesi kuwa timu hiyo inawania kuwasajiliA� Ismaila Diarra wa kilabu cha Rayon Sports na Ernest Sugira anayechezea timu ya AS Kigali inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Rwanda.