About Us

Radio Taifa ni kituo cha radio ambacho kinaheshimika zaidi humu nchini Kenya na katika ulimwengu mzima. Ni mojawapo was vituo vya radio vinavyomilikiwa na Shirika la Utangazaji compare and contrast essay guidelines la Kenya yaani Kenya Broadcasting Corporation (KBC). Radio Taifa ilianza kupeperusha matangazo mwaka wa 1953 kabla ya Kenya kuwa taifa huru na hasa kiliwalenga Wakenya Waafrika.

Radio Taifa inajivunia kuwa kituo pekee ambacho kimetekeleza wajibu muhimu mno katika kufanikisha maendeleo katika nchi hii, kuimarisha uzalendo na mshikamano wa kitaifa. Majina mengi mashuhuri katika siasa, michezo, uchumi, yalifikia umaarufu wao kutokana na kituo hiki. Je, na katika sekta ya utangazaji?

Radio Taifa ina watangazaji mahiri na wenye sifa kuu Watangazaji wanafahamu fika mahitaji ya wasikilizaji kuanzia habari, elimu na muziki wa kuburudisha. Hii ndio sababu kituo hiki kinawavutia wasikilizaji kutoka kila pembe ya Kenya. Isitoshe. Wakenya wanaoishi nje ya Kenya wanapokea matangazo yake yenye kuvutia kupitia mitambo ya kisasa na ndiposa umaarufu wake unaendelea kupanuka kila uchao.

Chunguza humu Kenya na nje ya Kenya na utabaini kuwa watangazaji wengi mashuhuri katika vituo vya utangazaji, vya runinga na radio, waliwahi kupitia Radio Taifa wakiwa wanafunzi au kama wafanyikazi. Kusema kweli Radio Taifa ndicho kituo pekee nchini Kenya kinachotoa nafasi kubwa zaidi kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kupata ujuzi wa utangazaji. Zaidi ya hayo, vituo mbalimbali vya utangazaji dunian hushirikiana na Radio Taifa baada ya kutambua informative speech on relationships sehemu muhimu ambayo kituo hiki kinashikilia katika taifa la Kenya.

Ni wazi kwamba msikilizaji haishi kwa muziki tu. Radio Taifa ambacho ni kituo kinachohimiza uzalendo kinatatambua kuwa elimu na habari ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya mtu binafsi na taifa letu. Kwa hivyo, Radio Taifa inatumia rasilmali zake nyingi kutayarisha vipindi kwa ajili ya wakenya; vipindi vya kilimo, teknolojia, michezo, dini na kisiasa.

Kituo cha Radio Taifa kina uwezo mkubwa wa kupeperusha matangazo ya moja kwa moja kutoka pembe yo yote ya Kenya. Radio Taifa inatumia teknolojia za kisasa kuhakikisha kuwa matangazo yake yanapatikana kupitia mitambo yote ya kisasa kama vile computer, rununu na runinga za digitali. Teknolojia hizi na ujuzi wa wafanyikazi na ushirikiano bora baina ya washika dau umewezesha Radio Taifa kuwa kituo cha kipekee nchini Kenya kinacholetea Wakenya majadiliano, moja kwa moja kutoka bunge la kitaifa na bunge la senate. Pia kituo hiki hukupeperusha shughuli muhimu za siku za kitaifa (Madaraka Day, Mashujaa Day, Jamhuri Day), michezo ya soka na riadha, na matokeo ya mitihani ya shule za msingi ( KCPE na ya shule za upili (KCSE).

Sikiliza Radio Taifa: Nairobi 92.9 FM, Mombasa 100.8 FM, Kisumu 104.5 FM, Nakuru 104.1 FM, Eldoret 88.6 FM, Namanga 89.9 FM, Meru 90.4 FM, Nyeri 87.7 FM, Kisii 103.3 FM, Malindi 90.1 FM, Kapenguria & Kitale 93.3 FM, Voi & Kibwezi 96.9 FM, Lodwar 88.6 FM, Lokichogio 89.3FM, Garsen 93.1 FM , Kitui & Kajiado 92.9 FM, Lamu 96.3 FM, Maralal 1107 MW, Wajir 1152 MW, Marsabit 675 MW, Garissa 567 MW.
Adult Search