Abba Moro Ashtakiwa Kwa Ufisadi Nigeria

Aliyekuwa waziri wa mashauri ya ndani wa Nigeria ameshitakiwa kwa kosa la ufisadi A�kufwatia A�mkanyagano uliotokeaA� wakati wa shughuli ya usajili wa watu wanaotafuta ajira,uliosababisha vifo vya watu 20.Abba Moro alikuwa msimamizi wa mpango huo,ambapo watu wasio na ajira ,hasa vijana kutoka vyuo vikuu walitakiwa kujisajili ili kupata ajiraA� kwenye wizara ya uhamiaji mnamo mwezi wa Machi 2014.Viwanja vya michezo vilivyotumika A�kama vituo kwa shughuli hiyo vilifurika watu na kusababisha mkanyagano uliosababisha maafa hayo.Hata hivyo Moro amekanusha mashtaka hayo kwenye kashfa hiyo ya takriban dola milioni 2.5 zilizokusanywa kama koto.Kuna kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini Nigeria,hasa miongoni mwa vijana.Mashtaka yaliowasilishwa na tume ya kukabiliana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha ilidai kuwa takriban vijana 675,000 walitapeliwa pesa zao kwenye shughuli hiyo,ambapo kila mwombaji alihitaji kulipa dola sita ili kusajiliwa kwa ajili ya kupatiwa ajira.