Kenya yakosoa ujumbe wa waangalizi wa EU

Serikali imeukosoa ujumbe wa uangalizi wa Umoja wa Ulaya kwa kutoa taarifa ya mwisho kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 huko Brussels, na kuitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha utaratibu. Taarifa ya ubalozi wa Kenya huko Brussels imesema Kenya haikufahamishwa kuhusu kutolewa kwa taarifa hiyo ukiongeza kwamba kwa kufanya hivyo waangalizi hao wa Umoja wa Ulaya EU hawakujali utaratibu wa taarifa ya maelewano iliyotiwa saini kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya jijini Nairobi hapo Juni 8 mwaka jana. Taarifa hiyo aidha ilisema hatua ya mwangalizi mkuu, Marietje Schaake, ya kutoa taarifa ya mwisho haikujali masharti ya ukiukaji wa taarifa ya maelewano kati yake na serikali ya Kenya kuhusu uangalizi wa uchaguzi na jumuiya hiyo iliyoitisha kuwepo kwa utaratibu na mwongozo rasmi. Ubalozi huo umetoa wito kwa uongozi wa bunge la Ulaya na Jumuiya ya UlayaA�A�kuchukua hatua na kuonyesha kujitolea kwa Jumuiya hiyo katika mkataba wake na washirika wake.

Schaake alisema ujumbe wa uangalizi wa Jumuiya ya Ulaya huko Brussels badala ya kutangaza taarifa yake humu nchini ulionelea ni vyema kutangaza taarifa hiyo huko Brussels kwa vile serikali haikuwa tayari kuwapokea.