Zanzibar yashinda Tanzania mabao mawili kwa moja

Timu ya soka ya Zanzibari ilitoka nyuma na kuishinda Tanzania mabao mawili kwa moja katika mechi yao ya pili ya kipute cha CECAFA, katika uwanja wa Gatuzi la Machakos. Zanzibari sasa inaongoza kundi a�?Aa�� kwa alama sita na imeratibiwa kupambana na Harambee Stars ya Kenya inayoshikilia nafasi ya pili kundini kwa alama nne, katika mechi yao ya tatu Jumamosi hii.

Tanzania ilikuwa inahitaji alama moja pekee ili kuhuisha azma yao ya kufuzu kwa mechi za mchujo, baada ya kutoka sare tasa na Libya katika mechi ya ufunguzi.A�A�Zanzibari iliishinda Rwanda mabao matatu kwa moja katika mechi yao ya ufunguzi Jumanne iliyopita. Tanzania ilienda kifuambele dakika ya 28 kutokana na bao la Himid Mao na kuongoza hadi mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Aidha, Zanzibari ilisawazisha bao hilo dakika ya 66 kupitia kwa Kassim Kahmis kisha Ibrahim Ahmada akaongeza la pili dakika ya 78. Zanzibari sasa inaongoza kundi a�?Aa�� kwa alama sita nayo Kenya ni ya pili kwa alama nne kutokana na mechi mbili. Katika matokeo mengine ya jana, Rwanda ilitoka sare kapa na Libya nayo Burundi ikailemea Ethiopia mabao manne kwa moja.