Watu 21 Wafa Maji Thailand

Watu 21 wamefariki baada ya mafuriko kukumba eneo la kusini mwa Thailand na kuathiri kilimo cha zao la mpira pamoja na muundo msingi. Zaidi ya familia nyingine elf 33 zimeachwa bila makao. Serikali imeanza kupeleka misaada ya chakula katika eneo hilo. Majira ya mvua nchini Thailand hukamilika mwezi Novemba na hivyo si kawaida kwa nchi hiyo kushuhudia mvua kubwa na mafuriko mwezi huu wa Januari. Mvua hiyo imenyesha katika mikoa 12 kati ya 67 nchini humo. Mnamo mwaka 2011, zaidi ya watu mia tisa waliangamia kwenye mafuriko ambayo pia yaliathiri sekta ya viwanda na uchumi wa nchi hiyo kwa jumla.