Claudio Bravo anawiri katika mechi ya kombe la mashirikisho

Mlindalango wa timu ya Manchester City, Claudio Bravo, alinawiri wakati Chile ilipofuzu kwa fainali ya kombe la mashirikisho duniani kwa kuishinda Ureno mabao matatu kwa moja kupitia mikwaju ya penalti.Bravo alizuia kiki za Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na NaniA� huku Chile ikifunga mikwaju yake mitatu. Chile sasa itachuana na mshindi baina ya Ujerumani au Meksiko, fainalini Jumapili hiiA� jijini St Petersburg.A� Bravo mwenye umri wa miaka 34 alisajiliwa na kocha Pep Guardiola kutoka Baselona msimu uliopita kuchukua nafasi ya Mwingereza Joe Hart. Ujerumani itachuana na Meksiko leo usiku katika mechi ya pili ua nusu fainali. Mechi hiyo itaoneshwa kenyekenye kupitia runinga ya KBC Channel One kuanzia saa tatu usiku, saa za Afrika Mashariki.